SportsCast
Kwanini kiwango cha Lukaku kimeshuka?
Episode notes
Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na assists 11 akiwa na klabu ya Inter. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni mifumo ya Chelsea, Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji. Prosper ameenda mbali zaidi kwa kuangalia aina ya pasi ambazo Lukaku anapokea pia maeneo anayokaa ili kupokea pasi. Episode hii imeelezea kila kitu kuhusu Romelu Lukaku.