SportsCast
By Clifford Sangai
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.
Latest episode
-
Washambuliaji wawili, mawinga wenye kasi na namba 10
Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili. Matumizi ya washambuliaji wawili Timu kuhamia back-four Mawinga wenye speed -
Chelsea ya Thomas Tuchel
Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG. Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina … -
Mwaka mmoja wa Nabi: Mbinu na Ufundi
Ni mwaka mmoja sasa tangu Nasreddine Nabi achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga kutoka kwa Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wake. Kuna mambo mengi ameyabadili katika kikosi hicho ambayo Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanayajadili … -
Taifa Stars ya Kim Poulsen
Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' -
Je, Carlo Ancelottii amebadilika?
Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo k… -
Falsafa ya Marcelo Bielsa
Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadi… -
Kwanini kiwango cha Lukaku kimeshuka?
Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na ass… -
Mikimbio ya Washambuliaji wa Simba SC
Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli? Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kucham… -
Arsenal: 'Pattern' ya ushambuliaji
Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongez… -
Kufeli na kufaulu kwa Viungo wa Simba na Yanga
Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo. Tumeang…